THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZAZI WAMESHAURIWA KUWALEA WATOTO WAO KATIKA MAADILI MEMA ILI TAIFA LIONDOKANE NA MATENDO MAOVU

Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Wazazi wameshauriwa  kuwalea watoto wao katika maadili mema ili Taifa liondokane na matendo maovu. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Madrasatul Musbah iliyopo Mtaa wa Nzasa na Kigoma manispaa ya ilala, Sheikh Kassim Mzee.

Akizungumza katika Tamasha la wazi kati ya Madrasa na Wazazi iliyoandaliwa na Madrasa hiyo, Sheikh Mzee amesema ni vyema watoto wakaandaliwa katika maadili mema mapema kama ambavyo wao wanafanya katika madrasa yao kwa kuwafundisha mambo mbalimbali kwa lugha ya kiarabu kwa lengo la kumjua Mwenyezi Mungu kwakuzingatia yale aliyoamrisha na yale aliyoyakataza.
Tamasha hilo la siku ya wazi kati ya Madrasa na Wazazi, Sheikh Mzee amefafanua kuwa wameamua kufanya tamasha hilo kwa lengo la kuwaonesha wazazi jinsi wanavyotakiwa kuwafundisha watoto wao (wanafunzi), ambapo wanafunzi hao wanaonesha kwa vitendo yale waliyokuwa wanajifunza darasani, nakudai  kuwa huo ni mwanzo ila watajitahidi kufanya matamasha  kama hayo kila mwaka, ili kuleta chachu kwa wazazi wengine kuona umuhimu wa kuwapa elimu watoto wao na kuwa watoto wema katika jamii ili Taifa liondokane na matendo maovu .
Wanafunzi wa madrasatul Musbah wakionyesha kwa vitendo namna ya kumuandaa maiti kabla ya kwenda kuzika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa katika tamasha la wazi kati ya Wazazi na Madrasa leo jijini Dar es Salaam.