Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amezitaka Halmashauri zote nchini kutekeleza agizo la kuunda Kamati za Watu Wenye Ulemavu kuanzi ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.

Mhe. Possi ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika mikoa ya Mwanza na Simiyu hivi karibuni ambapo alitembelea makazi ya watu wenye mahitaji maalum ya Bukumbi, Shule ya watu wenye mahitaji maalum ya Mitindo na kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi.

Kauli ya Dkt. Possi imekuja kufuatia maagizo yaliyolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka huu kwa kuziandikia Halmashauri zote kutekeleza uundwaji wa kamati za Watu wenye Ulemavu ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.

“Ni muhimu sana kutekeleza agizo lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwanzoni mwa mwaka huu ambalo limeeleza wazi kuundwa kwa Kamati za Watu wenye Ulemavu na ikumbukwe kuwa, suala hii lipo kisheria na lina miongozo yake katika utekelezaji wake”. Alisema Waziri Possi. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza jambo wakati wa ziara yake katika Shule ya wenye mahitaji maalumu ya Mitindo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Mwalimu wa wasioona Bw. Mika Sholla wakati wa ziara yake katika shule ya Mitindo Wilayani Misungwi Mwanza. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Ofisi ya Kituo cha Kulelea Watu wenye mahitaji maalum cha Bukumbi Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza wakati ya ziara yake.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mitindo pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali wakati wa ziara yake shuleni hapo Jijini Mwanza. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...