THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAHAKIKI WASTAAFU MKOANI DODOMA

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango, imezindua zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma mkoani Dodoma.
 Lengo la kufanyika kwa zoezi hili ni kuhuisha orodha ya malipo ya Wastaafu kwa mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika mwaka 2014.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Stanslaus Mpembe, alisema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku tano katika Kanda ya Kati ambayo imejumuisha mikoa mitatu ya  Morogoro, Dodoma na Singida.

Mpembe alisema lengo la kufanyika kwa zoezi hilo ni kubaini mabadiliko ya taarifa za Wastaafu kama vile kufariki ili kuepuka kulipa Wasiostahili.

‘Zoezi hili linafanyika kutokana na utaratibu uliojiwekea Wizara kufanya uhakiki wa Wastaafu baada ya muda fulani, zoezi hili litafanyika nchi nzima. Mpembe alisema’.

Aliongeza kuwa zoezi hilo litaisaidia Serikali kuhakikisha Wastaafu wote wanapata haki zao na kwa wakati. Aidha alitoa wito kwa Wastaafu kujitokeza kwa wingi kuhakikiwa ili waweze kupata haki zao za msingi, bila kusahau viambatanisho wanavyotakiwa kuwa navyo ili kurahisisha zoezi hilo.

Naye Katibu wa Chama Cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto aliishukuru Serikali kwa kuwajali na kukubali ombi lao kuhusani Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji  kwa kufikisha ombi lao walipofanya nae kikao la kulipwa mafao yao kila mwezi badala ya kila baada ya miezi mitatu.

‘Niwaombe Wastaafu wenzangu wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo ni la kwa faida yao. Kanyeto aliongeza’.

Kwa upande wa mstaafu Bi. Halima Matonya alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na ameipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwakumbuka, na amewapongeza  pia Waratibu wa zoezi hilo kwa kujipanga vema na kutoa maelekezo vizuri hivyo kufanya zoezi hilo kuchukua muda mchache.

Tayari zoezi kama hilo la uhakiki wa wastaafumwanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango limefanyika katika Kanda za Pwani na Nyanda za Juu Kusini ambapo ilijumlisha mkoa wa Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Katavi, Ruvuma, na Songwe.

Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kanda ya kati, zoezi hilo litaendelea katika Kanda ya Kaskazini ambapo litajumuisha Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga.
Mstaafu Christina Mashamba (kushoto), akifanyiwa uhakiki na Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Mmanispaa ya Dodoma, kushoto ni Jestina Naftaz na kulia ni Devotha Masanja.
Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao ya kuhakikiwa jijini Dodoma.