THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania yajivunia kuutangaza Utalii wa Tanzania kupitia 'Vintage Rally'

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imesema itaendeleza jukumu la kuutangaza Utalii wa ndani ya Tanzania nje ya mipaka yake ili kuwawezesha wataalii wengi kuja nchini na kuongeza pato la taifa. 

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti mara baada ya kuwasili jumla ya ndege 22 za kizamani zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na 1930 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana.

Corsaletti alisema kuwa jukumu la kuutangaza utalii wa Tanzania halipo kwa serikali pekee, kwani hata wadau wanafursa ya kufanya hivyo ili kuendelea kuleta tija nchini.

Alisema kuwa jumla ya marubani 48 kutoka ndege 22 wameshiriki katika mashindano ya ndege za zamani maarufu kwa jina la “ Vintage Air Rally” yenye lengo la kuutangaza utalii nchini na ushiriki wao mbali ya kujitangaza, pia ni sehemu ya kushiriki katika kazi za kijamii kwani mashindano hayo pia yanachangisha fedha kwa ajili ya shughuli za Unicef, Bird Life International na Seed Bombing.

“Mbali ya marubani na waongoza ndege, pia kuna washiriki wengine ambao wameambatana na ndege hizi kwa ajili ya kazi mbalimbali, hao wote watashindana katika hifadhi na kuona vivutio vya utalii na kwenda kuvitangaza nje ya nchi, hii ni fursa pekee ya kuvitambulisha duniani,”

“Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeshiriki ipasavyo kuhakikisha ndege zote zinapata mafuta ya kutosha aina ya Avigas mbayo kampuni yetu pekee ndiyo inazalisha mafuta haya ambayo ni ya ubora wa hali ya juu, mbali ya kupita katika mbuga ya Ngorongoro na kujionea utititiri wa wanyama na vivutio mbalimbali, baada ya hapo watapita Dodoma, Songwe (Mbeya) kabla ya kuelekea Zambia,” alisema Corsaletti. 

Wafanyakazi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi, Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya marubani wa ndege za kizamani mara baada ya kuwasili Zanzibar.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy  Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza  katika hafla maalum baada ya kuwasili  jumla ya ndege 22 za kizamani  zilizotengenezwa kati ya miaka 1920 na  1930 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar jana.
 Mwenyekiti wa bodi ya Puma Energy  Tanzania,  Dk Ben Moshi (wapili kushoto)  akisalimiana na rubani pekee wa kike  katika mashindano ya kurusha ndege za  kizamani zilizotengenezwa kati ya mwaka  1920 na 1930 mra baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid  Amani Karume, Zanzibar, wa kwanza kushoto  ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya  Utalii Zanzibar, Dk Miraj Ussi na wa pili  kulia ni Meneja Mkuu wa Puma Energy  Tanzania, Dk Ben Moshi.
Moja ya ndege ya kizamani iliyotengenezwa kati ya miaka 1920 na 1930 ikiwasilikwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika moja ya mashindano ya ndege hizo yajulikanayo kwa jina la "Vintage Air Rally" yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania. 

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya  Utalii ya Zanzibar, Dk Miraj Ussi  akizungumza katika hafla ya kuzipokea  jumla ya ndege 22 za kizamani  ziliyotengenezwa kati ya miaka 1920 na  1930 mara baada ya kuwasili kwenye uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume katika moja ya mashindano ya ndege  hizo yajulikanayo kwa jina la "Vintage Air  Craft Rally"

HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA