Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam.
Kampuni
moja ya Ujerumani ya Ferrostaal, inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha
mbolea katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, kitakacho gharimu zaidi ya
Euro Bilioni 1 nukta 2 (1.2bln) ambacho kinatajwa kuwa kitakuwa moja ya
viwanda vikubwa vya mbolea Barani Afrika.
Hayo
yamesemwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, EGON KOCHANKE, wakati
alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, Jijini Dar es salaam, ambapo wawili hao wamezungumzia
masuala kadha wa kadha yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani
uliodumu kwa muda mrefu.
Balozi
Kochanke amesema kuwa kiwanda hicho kitakachojengwa kwa ubia kati ya
kampuni hiyo ya Ujerumani na wawekezaji wazawa na wengine kutoka Bara la
Asia, inatokana na hamasa kubwa ya serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhamasisha ujenzi wa
viwanda.
“Kiwanda
hiki kitakuwa kikubwa zaidi ya mara mbili ya kiwanda cha saruji cha
Dangote kilichoko Mtwara na kitagharimu Euro Bilioni 1.2, kitasisimua
uchumi wa nchi pamoja na kukuza ajira” alisema balozi huyo aliyeambatana
na naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, John Reyels na Mkurugenzi wa
Ushirikiano wa nchi hiyo Julia Hannig.
“Mbali
ya Kampuni hiyo ya Ferrostaal, wawekezaji wengine ni kampuni ya Mbolea
ya Minjingu, na kampuni nyingine kutoka Pakistan ambayo kwa pamoja
wameingia ubia wa kujenga kiwanda hicho cha mbolea kitakachokuwa
uwekezaji mkubwa” Aliongeza Balozi Egon Kochanke.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi. Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...