WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia sasa, Serikali imekwishaipatia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sh. bilioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Amesema hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba iliyokuwa inazikabili hospitali mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Desemba Mosi, 2016) wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Manyara aliposimama wilayani Babati akiwa njiani kwenda Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku saba inayotarajiwa kuanza kesho.
Amesema suala la dawa kwa sasa linaenda vizuri, hivyo amewataka viongozi wa mikoa kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinavyopelekwa katika hospitali zao zinatumika kama ilivyokusudiwa.

“Suala la dawa linaenda vizuri sasa. Hakikisheni mnadhibiti mianya ya upotevu wa dawa kwenye hospitali zetu kwa kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wa sekta ya afya wasiokuwa waaminifu,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuweka utaratibu wa kujenga hospitali ya rufaa ya mkoa pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuwawezesha kupata huduma ya matibabu bure kwa mwaka mzima.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuachana na mila potofu na badala yake wawasomeshe watoto wao hasa wa kike kwani suala la elimu mkoani Manyara bado halijapewa kipaumbele.

“Hakikisheni watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza wanakwenda shule ifikapo Januari. Maofisa Elimu shirikianeni na halmashauri kuhakikisha jambo hili linafanikiwa kwaasilimia 100,” amesema.

Akizungumzia kuhusu suala la utoro na mimba kwa watoto wa kike, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kudhibiti jambo hilo kwa kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera  na Katibu Tawala wa Mkoa  huo , Eliakim Maswi  (kulia) wakati  aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba 2, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba2, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...