Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

TIMU ya JKT Ruvu imefanikiwa kunasa saini ya kocha wa timu ya Vijana Chini ya miaka 17 Serengeti Boys Bakari Shime na kumpatia kandarasi ya miaka miwili ili kuweza kukinoa kikosi hicho cha maafande.

Shime amechukua nafasi ya Mzanzibar Malale Hamsini aliyekuwa anakinoa kikosi hicho raundi ya kwanza lakini akishindwa kuipatia matokeo timu hiyo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa JKT Ruvu Kocha mwandamizi Abdalla Kibadeni amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya uongozi wa juu kuona kuwa Kocha Malale Hamsini ameshindwa kuipatia matokeo timu yake na kama raundi ya pili ikiendelea hivyo basi inaweza ikashuka daraja.

Kibadeni amesema kuwa, kwa sasa Shime amepewa nafasi ya kuangalia wachezaji wa timu ya vijana kuangalia kama anaweza kuwatumia kwani hawana malengo ya kufanya usajili wowote kwa wachezaji kutoka timu zingine.A

Shime ameweza kufanikiwa kufanya vizuri na timu ya vijana ya Serengeti Boys kwahiyo wana imani naye kuweza kuisaidia timu ya JKT Ruvu katika duru la pili ambapo kwa sasa ipo nafasi ya tatu kutoka Chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...