THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAHITIMU CHUO KIKUU MUHIMBILI WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

Zainab Nyamka, Globu ya Jamii .

MKURUGENZI wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu amesema kuwawanafunzi wanaohitimu wanatakiwa kwenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kutokuacha kujiendeleza na kujifunza kwani dunia inabadilika na magonjwa yanazidi kujitokeza kila siku.

Aliyasema hayo, wakati wa kongamano la Mjasiri lililowakutanisha wanafunzi waliosoma zamani katika Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na wanafunzi wanaohitimu na kuwataka kuendelea na utafiti wa magonjwa mbalimbali yanayowazunguka jamii.

Prof Temu amesema kuwa MUHAS wameweza kufanya kitu kizuri sana kwa kuwakutanisha wanafunzi waliomaliza hapa na mkusanyiko huu utasaidia kuweza kuleta mawazo mapya na zaidi yatasaidia kwenye kukuza na kuendeleza sekta ya afya.

"kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, tunaoenda kuwapongeza sana MUHAS kwa jitihada nzuri waliyofanya ya kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma pamoja na hawa wanaohitimu katika ngazi mbalimbali kwani tunachokijua ni kuwa watabadilishana uwezo hasa kwa wale waliokuwa washapata uzoefu wa muda mrefu,"amesema Prof Temu.

Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya amesema kuwa  kongamano hili la Majasiri litaleta manufaa makubwa sana kwani kutawawezesha wanafunzi wanaohitimu na waliomaliza miaka ya nyuma kufanya kazi kwa pamoja, kwani Majasiri wanachangia kwa kiwango kikubwa katika Chuo kwa kutoa mawazo na hata fedha kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya chuo.

Kaaya amesema kuna changamoto nyingi sana  katika kuendeleza maendeleo ya chuo hususani kwa upande wa fedha ila kwa kuwakutanisha hawa Majasiri kutasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye kutatua matatizo ya chuo cha MUHAS.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Joyce Ndalichako wakati wa Kongamano la Majasiri wa Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kushoto ni
Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya, Mwenyekiti wa kamati ya Chuo Mariam Joy Mwaffisi, kutoka kulia ni makamu mwenyekiti wa kongamano Dr Ellen Senkoro na Mwenyekiti wa wa kongamano hilo  Prof Charles Mgone.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akiangalia baadhi ya maonesho yaliyoandaliwa na Wahitimu wanaomaliza kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Prof Silvia Temu akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya (kushoto),  Mwenyekiti wa wa kongamano la Majasiri wa Chuo hicho Charles Mgone.
 Baadhi ya wahitimu na wahitimu wakiwa makini kufuatilia kongamano hilo. Picha zote na Zainab Nyamka.