Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, ameiagiza Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) kuwachukulia hatua wale wote wanaoitia doa taaluma hiyo kwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

Maagizo hayo yametolewa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango, wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) uliokwenda sambamba na ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa wahasibu unaojumuisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema kuwa Idadi ya Wahasibu wenye sifa inazidi kuongezeka na hivyo kuisaidia Serikali, japo kuwa Serikali hairidhiki kuona wanataaluma wa Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (CPA) wanaongezeka huku vitendo vya ubadhilifu wa fedha za Umma na ufisadi vikiendelea kuripotiwa.

“Wapo hata wahasibu wanaotumia taaluma yao vibaya, wanaowawezesha wafanyabiashara kukwepa kodi, wanachakachua vitabu vya taarifa za fedha na kufanya ufisadi kwa njia ya kalamu na kompyuta jambo ambalo halikubaliki hata kidogo” Aliongeza Dkt. Mpango

Amesema kuwa machozi ya masikini wa Tanzania yatawafuata mafisadi hadi kaburini lakini serikali ya Awamu ya Tano haitasubiri hao mafisadi wafe, itawatumbua na wala hakuna mzaha na kwamba tayari mahakama ya mafisadi imeanza kazi na itawashughulikia.   

Aidha, Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaasa wanataaluma wa uhasibu na ukaguzi wa hesabu kuitumia taaluma yao kuisaidia Serikali katika hatua yake ya kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda kwa kuwa taaluma hiyo ina umuhimu mkubwa.
 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

 Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
 Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...