Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wananchi mapema leo asubuhi katika Uwanja wa Ushirika wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoezi ya pamoja kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la makamu wa rais Samia Suluhu Hassan la kutenga siku moja kwa ajili ya mazoezi kila mwezi, ambapo amesema kuwa amekabidhi orodha ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, na siku ya jumatatu yatatangazwa. Amesema yapo majina 42 ya washukiwa wa biashara hiyo ya dawa za kulevya mkoani humo na Watuhumiwa watano kati yao watasifishwa mahakamani siku hiyo hiyo. Anasema waliokurupushwa Dar sasa wanataka kuhamishia mapito yao Kilimanjaro, Ametoa onyo wasijaribu kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kupambana nao. Na Dixon Busagaga, Globu ya Jamii - Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...