Mahakama kuu ya Tanzania imesema itafanya mpango wa kuongeza kasi ya utoaji wa haki kwa watu wote ikiwemo kupunguza  kesi za zamani katika ngazi zote za mahakama nchini.
Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma katika kilele cha maonyesho ya wiki ya sheria, akisisitiza watongeza vitendea kazi na watumishi wa mahakama ili kuwepo na urahisi katika mfumo wa kusikiliza kesi na kuzitolea hukumu.
Akizungumzia baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na mmoja wa wananchi Profesa Juma amesema kuwa wamepokea malalamiko juu ya mahakama moja ambayo hakuitaja jina lake ambayo watumishi wake wamekuwa wakitoa lugha chafu,uzembe,kuchelewesha haki,kutumika kama vishoka sambamba na kuongea lugha za jazba hali ambayo ilimkwaza mwananchi huyo.
‘’Natoa rai kwa mahakama kuhakikisha wanatoa takwimu nawakumbusha kwamba kuna waraka wa Jaji Mkuu wa mwaka 2013  ambao aliwataka Majaji wafawidhi,Majaji wafawidhi na watendaji kuona kila baada ya miezi mitatu kuanzia Julai 2013 kuwasilisha mashauri ya  muda mrefu’’.amesema Profesa Juma.
 Pia ametoa rai kwa wadau wote kuendeleza yale mazuri yaliyojitokeza katika wiki ya huduma za kisheria katika viwanja vya mnazi mmoja ikiwemo kusikiliza kero za kisheria zinazowakabili wananchi hata watakapofika katika ofisi zao.
 Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akizungumza katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jijini  Dar es Salaam.
 Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akimkabidhi laptop Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe. Asia Mjemah kwa ajili ya uchapishaji nakala za hukumu jana  jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jiji Dar es Salaam

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa,Ibrahimu Juma akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mblimblia katika viwanja vya Mnazi  mmoja leo jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...