Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi leo umezindua kampeni ya upandaji miti katika Wilaya ya Kahama ikiwa na lengo la kupanda mti kwa kila wakia ya dhahabu ambayo imechimbwa kwenye mgodi wa Buzwagi, ambapo miti zaidi ya milioni moja na laki sita inatarajiwa kupandwa katika kipindi cha miaka miwili.
Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa hatua hiyo na kusema ni ya kizalendo kwa kuwa itasaidia katika kuboresha hali ya mazingira ya wilaya ya Kahama.
“Jukumu la upandaji miti na kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa ni letu sote, Wenzetu wa Buzwagi wameanza kuonyesha jitihada kwa kupanda miti milioni moja na laki sita, hivyo sote kama Jamii hatuna budi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha kila mmoja wetu katika eneo lake anapanda miti na kuifanya wilaya yetu ya Kahama izidi kupendeza”Alisema Nkurlu.
Akizungumzia Malengo ya Kampeni hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo amesema kama wadau muhimu wa mazingira wanalojukumu la moja kwa moja kuhakikisha shughuli za utunzaji wa mazingira zinakuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.

Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayopandwa katika maeneneo mbalimbali wilayani kahama kwa lengo la kutunza mazingira pamoja na kuufanya mji wa Kahama upendeze.
Mkuu wa wilaya kahama Fadhili Nkurlu akimwagia maji mti alioupanda wakati alipozindua kampeni ya upandaji miti
Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Mussa Mchenya akishiriki pia upandaji miti.
Afisa Usalama wa Wilaya ya Kahama Aretus Lyimo akishiriki upandaji miti wakati wa zoezi la uzindunzi wa upandaji miti milioni moja na laki sita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...