Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBC,
Mongateko Makongoro (mwenye suti nyeusi) akipiga picha ya pamoja na washindi wa
tuzo ya utoaji wa mikopo binafsi walioingia kwenye Kundi la Watu Mashuhuri wa
NBC lijulikanalo kama ‘ ‘Kundi la Shilingi Billioni Moja’. Tuzo hizo zilitolewa
kwenye sherehe maalum ya kuwatunuku
watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi
karibuni.
Mkurugenzi wa Huduma Reja Reja
za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), akipiga picha ya pamoja na
baadhi ya wafanyakazi bora waliofanya vizuri katika mwaka 2016 walio chini ya kurugenzi
yake, katika sherehe maalum ya
kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kushoto), akionyesha cheti alichotunukiwa mara baada ya kutangazwa meneja bora wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja wa amana za wateja NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), akikabidhi kombe la ushindi kwa Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff baada ya tawi hilo kuibuka kidedea katika kutoa huduma za kibenki kwa wateja wa akaunti ya malengo kwa mwaka 2016 . Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...