Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo 31 Januari 2017, wamekutana na wadau wa mafuta katika kuangalia fursa za uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini ambapo kwa sasa pia wanaangalia fursa za kutumia bandari ya Tanga ili kusaidia wananchi wa Mikoa ya Kaskazini.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Wakala Mkuu wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja wa (PBPA) Modestus Lumato wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Lumato amesema kuwa, kwa sasa PBPA inaangalia kushusha mafuta katika bandari ya Tanga ili kupunguza msongamano kwa bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuondoa foleni..

Amesema mwezi uliopita wameanza kushusha mafuta bandari ya Tanga kwa kiwango kidogo kutokana na ukubwa wa eneo la awali, ambapo kwa sasa tenda inayofuata wanatarajia kushushia tena Mkoani Tanga kwani itasaidia wateja wao wa ukanda wa Kaskazini ikiwemo mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na mikoa mingine ya jirani.

“Tani za mafuta ya Dizeli na Petroli zinatarajiwa kwa awamu ijayo tukashuka bandari ya Tanga kwa kuanzia na tani 45,000. Mikoa ya Mwanza na jirani na mikoa hiyo itanufaika kwa kuja kuchukua bidhaa hiyo Tanga na kuliko kuja Dar es Salaam.” Alieleza Modestus Lumato.

Amesema kuwa wameshatangaza zabuni ambapo wamejitokeza wazabuni watatu katika zabuni hiyo iliyotangazwa .
 Kaimu Mkurugenzi wa wakala waagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) Modestus Lumato  wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, 
 
Sehemu ya wadau wakifuatilia mjadala huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari,

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...