THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Hali ya Mzee Haji Gora Haji mtunzi wa ‘Mpewa Hapokonyeki’ ilivyo sasa...

Na Salum Vuai, MAELEZO - Zanzibar
JUMATATU ya tarehe 27 Machi, 2017, niliamua kuakhirisha mambo yangu mengine yaliyokuwemo kwenye ratiba yangu na kuamua kufunga safari hadi mtaa wa Chumbuni, Wilaya ya Mjini Unguja.

Nia yangu ilikuwa kwenda kumjulia hali msanii mkongwe wa Zanzibar, Mzee Haji Gora Haji (pichani), ambaye kwa miezi kadhaa sasa nyendo zake zimekatika kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Gwiji huyu wa sanaa mbalimbali ikiwemo ushairi, uandishi wa vitabu vya hadithi fupi, tenzi na mashairi ya nyimbo, ni miongoni mwa watu muhimu katika historia na tasnia ya usanii hapa nchini.

Kwangu mimi, na ninaamini kwa wengine wanaopenda sanaa, Mzee Gora aliyezaliwa mwaka 1933 kijijini Tumbatu, ni mwalimu na mlezi katika kuwafinyanga washairi chipukizi na wa makamu ambao bado wanaendelea kujifunza kwa kuamini kwamba sanaa ni utamaduni endelevu unaokuja kivyengine kadiri siku na mambo yanavyobadilika.

Ingawa nilikuwa nikipanga kumtembelea siku nyengine isiyokuwa tarehe 27 Machi niliyoitaja awali, lakini nililazimika kubadili mpango huo na kuamua kuwahisha ziara yangu hiyo kutokana na jambo maalumu liliougusa mtima wangu usiku wa Machi 26, mwaka huu.
Ni jambo gani hilo? Endelea kusoma makala haya mstari kwa mstari, neno kwa neno, herufi kwa herufi ili ulijue.