Wateja wa mtandao wa mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, kuanzia leo wataanza kunufaika na programu mpya  na ya kisasa zaidi katika kufanya miamala yao kupitia huduma ya M-Pesa ambayo itawezesha watumiaji wa huduma hii wenye simu za intanenti kuifurahia zaidi kwa kuwa imerahisishwa na kuboreshwa zaidi.

Programu hii inawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pesa kufanya mihamala kwa haraka bila kufuata mlolongo mrefu wa programu ya awali - kwa mfano mtumiaji anaweza kuangalia akiba ya salio lake kwa kubonyeza mara moja maelekezo ya kupata huduma hii bila gharama yoyote.Pia programu hii imekuja na mfumo wa kufanya mihamala ya malipo kwa teknolojia ya kisasa na haraka inayomrahisishia maisha mtumiaji.

Katika programu hii mpya pia inawezesha mteja kuona jina la wakala au jina la kampuni au biashara kabla ya kutoa au kutuma hususani katika mihalama ya kulipa kwa kutumia huduma ya Lipa kwa M-Pesa.

Mkurugenzi wa huduma za biashara kwa njia ya mtandao wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit,amesema kuwa  programu hii imezinduliwa rasmi leo baada ya kufanyiwa utafiti  katika soko na kujiridhisha kuwa italeta mapinduzi ya matumizi ya kufanya mihamala ya fedha kwa M-Pesa kwa kuifanya kuwa rahisi zaidi kwa watumiaji hususani wanaotumia simu za intanenti (Smart Phones).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...