Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa jalada la kesi  ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya bilioni 1.16 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lipo kwa  (DPP)

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, amesema kuwa, jalada hilo liko kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya upelelezi uliofanyika

Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage  ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20,2017 kwa ajili ya kutajwa. 

Maimu anashtakiwa pamoja na  Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.

Wengine ni Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Wanakabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya milioni 1,169,352,931.

 Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kati ya  Januari 15 hadi 19,  mwaka 2010 katika makao makuu ya NIDA   wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wanadaiwa kuidhinisha malipo kwa Gotham International Limited (GIL) ya Dola za Marekani 2,700,00 bila ya kutumia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilivyowekwa na BOT.

Aidha wanadaiwa kuidhinisha malipo ya USD 1.8 kwa  GIL bila kuzingatia viwanjo vya fedha.


Ilidaiwa kuwa, Juni 20, 2014, waliidhinisha USD  675,000 kwa GIL bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha, hivyo kuifanya kampuni hiyo kupata faida ya Sh 42,471,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...