Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi katika utengenezaji wa vyombo vya Moto ya Mahindra yenye Makao Makuu yake Mjini New Delhi Nchini India imeamua kuiunga Mkono Zanzibar katika muelekeo wake wa kuimarisha miradi ya maendelelo.
Mkuu wa shughuli za Kimataifa wa Kampuni hiyo Bwana Arvind Mathew alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni yake na Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilichofanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Mjini New Delhi. 
Bwana Arvind Mathew alisema kutokana na kukuwa kwa Teknolojia ndani ya Kamupuni ya Mahindra, Uongozi wa Taasisi hiyo ya Uhandisi Nchini India hivi sasa umekusudia kuelekeza nguvu zake katika Mataifa rafiki kwa nia thabiti ya kuona Mataifa hayo hasa yale ya Bara la Afrika yanakuwa Kiuchumi. 
Alisema Mahindra imejipanga kuangalia njia za kusaidia uimarishaji wa Sekta ya Kilimo kupitia miundombinu imara na vifaa vya Kisasa vitakavyoongeza nguvu za uzalishaji kwa kundi kubwa la Wakulima katika mazao ya viungo yenye tija kubwa katika soko la Kitaifa na Kimataifa. Alisema Wataalamu wa Kampuni ya Mahindra wamekuwa shahidi katika safari zao za kawaida kwenye Mataifa mbali mbali waliyowekeza miradi yao ya Kiuchumi kuwaona Wakulima wa maeneo hayo wakiendesha shughuli zao katika mazingira magumu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa ili kutoka Kushoto akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mji wa New Delhi Nchini India kwenye Makamo Makuu wa Shirikisho la Viwanda Mjini New Delhi. Wa kwanza kutoka Kulia ni Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya Mahindra Bwana  Arvind Mathew, wa kwanza kutoka Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mamboya na Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mh. Mihayo Juma N’hunga.
 Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya Mahindra Bwana  Arvind Mathew Kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
 Balozi Seif  akizungumza katika kikao cha pamoja mkati ya Ujumbe wake na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Mji wa New Delhi na Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo makamo Makuu ya Shirikisho la Viwanda la India Mjini New Delhi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila na Kulia yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bibi Asha Ali Abdulla.
 Balozi Seif akimzawadia mlango Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila mara baada ya kumaliza mazungumzo yao 
Picha na – OMPR – ZNZ. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...