Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yamewakutanisha wahariri ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kujadili namna ya kufanya kazi pamoja na mashirika hayo. Mashirika ya umoja wa mataifa yaliyoshiriki kwenye mkutano huo ni UNDP, ILO, FAO, WFP, UNHCR, UN Women, nk.

Akizungumza na wahariri Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema umoja wa mataifa uko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kuonesha mchango wao kwenye jamii. Hivyo mchango wa waandishi wa habari ni wa msingi kwao na ili kuweza kutekeleza malengo waliyojiwekea hasa kuinua uchumi wa Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akifungua mafunzo kwa wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya akizungumza jinsi wanavyoshirikiana na serikali ya Tanzania pindi wanapoingia wakimbizi kutoka nchi mbalimbali zinazoizunguka nchini ya Tanznaia hasa zile nchi zenye migogogro ya kisiasa.

Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu, akitolea ufafanuzi baadi ya mambo kwenye mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena akiwasilisha mada  kuhusu mazingira wanayofanyia kazi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu jukwa la wahariri Tanzania linavofanya kazi hasa kwenye habari za jamii kwenye mkutano wao pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...