THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MBUNGE MSTAAFU WA TEMEKE ABBAS MTEMVU AFUNGUA MKUTANO WA VICOBA NA BENKI YA KIISLAMU YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya Maofisa wa Benki ya Kiislamu ya Amana, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wa wanachama wa Vicoba wa Wilaya ya Temeke na benki hiyo, mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, alipoufungua mkutano wao mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki hiyo, Munir Rajab.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati wa ufunguzi, wa mkutano wao, ukumbi wa PTA, Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Amana, Munir Rajab na wa kwanza ni Mkuu wa Masoko wa benki  hiyo, Dassu Mussa.