THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Mtanzania Dkt Harun Nyagori Apatiwa Tuzo ya Heshima ya magonjwa ya moyo nchini Marekani

Daktari Bingwa Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Moyo Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Fransisco, Dkt Harun Nyagori, ametunukiwa  Tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE OF CARDIOLOGY) na Kutambuliwa na Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo jijinin Washington DC, Marekani,  leo.
Akiongea baada ya kupokea zawadi  hiyo kwa njia ya simu  Dkt Nyagori anasema leo ilikuwa ni siku pekee ya Kuonyesha Ulimwengu kwamba Tanzania pia inaweza na kwa kutimiza ndoto yake ya kuipatia Heshima Tanzania ili itambulike  kuwa ina Wataalamu wanaoweza kufanya Utafiti Mbali mbali wa Maradhi ya Moyo.
Dkt Nyagori amepongezwa sana na Watanzania na Wanasyansi mbalimbali Nje na ndani ya nchi. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Daktari wetu na wanataalauma Mbalimbali walioonyesha mfano kama Daktari wetu huyu. 

Dkt Harun Nyagori akipozi baada ya kutunukiwa  tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE CARDIOLOGY)  toka  Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo mjini Washington DC, Marekani,  leo. 
Dkt Harun Nyagori akipongezwa baada ya kutunukiwa  tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE CARDIOLOGY)  toka   Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo mjini Washington DC, Marekani,  leo.