Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema  kuna athari kubwa za kutotoa taarifa muhimu na za wazi zinazohitajika na wananchi hivyo kuwanyima haki ya kujua utendaji wa Serikali.

Waziri Nape alisema kwa sasa utoaji wa habari na taarifa za Serikali kwa umma si utashi tena wa Afisa Habari au kiongozi wa Ofisi ya Umma bali ni matakwa ya kisheria ambayo yamewekewa kanuni na misingi katika Sheria za Huduma ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa  za 2016.

“Kwa sasa kutoa habari zilizo wazi tena kwa wakati, sio utashi wa mtu tena bali  ni matakwa ya Sheria  hivyo ni wajibu wa kiongozi kutoa taarifa kwa umma” alisisitiza Waziri Nape.

Aidha alisema kuna baadhi ya Maafisa Mawasiliano ambao mpaka mwaka unakwisha hawajawahi kuandika taarifa yoyote kwa umma wala kutoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa Serikali hivyo kuijengea Serikali taswira mbaya kwa Wananchi.

“Katika awamu hii hakuna “Mungu Mtu” katika utoaji wa taarifa hivyo ni wajibu wa viongozi kutoa taarifa au ufafanuzi pale inapohitajika na sio kukwepa waandishi wa habari, na kutofuatilia kero za Wananchi ” alisema Waziri Nape.

Waziri Nape aliwataka Maafisa Mawasiliano na Viongozi katika Taasisi za umma nchini kutekeleza Sheria ipasavyo kwa kutoa habari na taarifa kwa umma bila urasimu.

“Ndugu zangu msikalie taarifa maana kama hutoi ushirikiano kwa wana habari na wote wanaohitaji taarifa watatunga zakwao ,hapo sasa mnaanza kukimbizana kukanusha” ,Alisisitiza Waziri Nape.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...