THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NMB Mobile TISS Kumaliza Tatizo la Foleni kwa Wateja

Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanahabari kuzinduwa huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.[/caption] NMB imezindua rasmi huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS), kutoka katika akaunti za benki hiyo, kwenda kwenye akaunti za benki nyingine, sambamba na kufanya manunuzi na malipo. 

NMB Mobile TISS, ni huduma ya kwanza kutolewa na benki nchini Tanzania, ambayo imetajwa kuwa ni njia rahisi, salama na ya haraka katika mchakato wa kutuma ama kuhamisha fedha kutoka NMB kwenda benki nyingine.

 Akizungumza katika hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa wanahabari, Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili alisema NMB Mobile TISS ni mwarobaini wa wateja wao kutumia muda mrefu kwenye foleni za kuhamisha ama kutembea na fedha mkononi. “Huduma hii inakuja kumaliza tatizo la wateja kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, tumekuja na huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo. Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili (mwenye suti ya bluu mbele) akizungumza na wanahabari kuzinduwa huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.

Aliongeza ya kwamba, NMB Mobile TISS haiishii tu katika kuhamisha fedha kutoka akaunti ya NMB kwenda benki nyingine, bali inaenda mbali na kupokea ama kutuma miamala ya mitandao ya simu za mkononi. Huduma hiyo inayoweza kutumiwa na wateja wa NMB Mobile, inapatika na kwa mteja kubonyeza alama nyota, kishanamba 150, alama ya nyota, kisha namba 66 na mwisho alama ya reli na kufuata maelekezo (*150*66#).

Naye Geofrey Mwijage, ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, lisema benki yake imejidhatiti vya kutosha katika kutanua huduma miongoni mwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla. Alisema NMB Mobile TISS inaenda kuwa mshirika sahihi wa Watanzania, katika kuharakisha maendeleo yao na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kuelekea Tanzania ya Viwanda.