Picha ya mchoro wa binadamu wa kale wakitembea katika eneo la Laetoli lililoko km 45 kusini mwa Olduvai gorge. 
Na Geofrey Tengeneza- Berlin.

Nyayo na picha za michoro ya binadamu wa kale (zamadamu) zinazooneshwa katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya ITB yanayoendelea hapa Berlin Ujerumani sambamba na maelezo sawia ya historia yake inayotolewa na mhifadhi wa Paleontolojia (masalia ya kale) Dkt. Agnes Gidna kutoka Makumbusho ya Taifa Bi wakishirikiana na maafisa waandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania inawapagaisha maelfu ya wageni wanaotembela banda la Tanzania katika maonesho hayo.

Nyayo na michoro hiyo ya binadamu wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 4 iliyopita katika eneo la Laetori kilometa 45 kusini mwa Oldvai gorge pamoja na vielelezo mbalimbali vya vivutio kadhaa muhimu vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti n.k vimekuwa chachu ya kuvutia wageni wanaotembelea banda la Tanzania ambao pia wameonesha dhamira kubwa ya kuitembelea Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi pamoja na utangazaji mkubwa wa vivutio mbali mbali vya utalii vya Tanzania unaofanywa katika maonesho haya, TTB imeamua pia mwaka huu kuweka mkazo maalumu katika kuitangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu wa kale.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa wageni kuhusu vivutio mbalimbali vilivyopo Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya ITB.
Mhifadhi wa Masalia ya kale (Palentolojia) wa makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Gidna akitoa maelezo kuhusu historia ya binadamu wa kale pamoja na nyazo zake zilizo umbuliwa Laetori Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania .
Mtangazaji wa kituo cha Umma cha televisheni cha Ujerumani Bw. Hoeks akifanya mahojiano mubashara na Mhifadhi wa Palentolojia wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Digna mbele picha ya mchoro na nyayo za zamadamu ndani ya banda la Tanzania lililopo katika maonesho ya ITB Berlin Ujerumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...