Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.
Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.
Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.
Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.
Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.
“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.
“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi...Wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Machi, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akielezea changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisiliza changamoto za wakulima na wafugaji katika kjijiji cha Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Maggid Mwanga baada ya kuongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiongea nao katika kijiji cha  Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...