Mratibu wa Ubia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) Bi.Tullah Mloge akifafanua jambo wakati wa ziara ya kutembelea wakulima walionufaika miradi mbalimbali inayoratibiwa na SAGCOT hivi karibuni Mkoani Njombe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mwandamizi Msaidizi Mstaafu wa polisi, Bw. Zelote Stephen. Ziara hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kilimo na ufugaji kutoka Tanzania na Uholanzi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Bw.Zelote Stephen ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi Mstaafu (SAPC) ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kilimo na ufugaji kutoka Uholanzi mara baada ya kumaliza mazungumzo na ujumbe huo ulioonesha nia ya kuwekeza katika Mkoa wake. Kushoto ni Mratibu wa Ubia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT) Bi.Tullah Mloge na wapili kushoto ni miongoni wa wajumbe hao Bi.Carmen Breeveld. Pamoja na wadau wengine wa kilimo hivi karibuni.

MKUU wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amewavutia wawekezaji kutoka Uholanzi kwenda kuwekeza mkoani humo katika sekta za kilimo na ufugaji, akisema Rukwa ina fursa nyingi za uwekezaji.

Stephen ambaye pia ni Kamishna Mwaandamizi mstaafu wa Police (SACP), amewaambia wawekezaji katika sekta za kilimo na ufugaji kutoka Uholanzi kuwa mkoa wake una fursa nyingi za kilimo na ufugaji lakini hakuna wawekezaji wa uhakika waliothubutu kuendeleza fursa hizo.

Alisema uwekezaji zaidi katika sekta za kilimo na ufugaji, zitasaidia sana jitihada za mkoa wake za kwasaidia wakulima wadogo kuondokana na umasikini.

Wafugaji hao kutoka Uholanzi walishiriki Kongamano la Wabia na Wadau wa maendeleo ya Kilimo Kusini ya Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT Forum Partnership 2017) hivi karibuni na pia kwenye safari ya kujifunza (Learning Journey).

 “Nimeona zipo fursa nyingi tunaweza kuzipata kwa kushirikiana na wadau wa kilimo ndani na nje ya nchi ili kuongeza thamani ya mazao. Nitoe wito kwa wananchi wa Rukwa kuwa fursa inayokuja mkoani kwetu ni vema wajipange na kujiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kuwafikia, kuwahudumia na kunufaika kupitia kilimo na ufugaji,” alisema Bw. Stephen.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa wahabari, Bibi Carmen Breeveld, mfugaji kutoka Uholanzi ambaye aliongozana na wanawake wengine wawili katika ziara hiyo ya mafunzo mkoani Njombe ambapo waliona namna ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na nguruwe unavyofanyika nchini.

“Tunataka kumuunganisha Mkuu wa Mkoa (Rukwa) na Serikali ya Uholanzi na sekta binafsi ili kuondoa matatizo yanayowakabili wafugaji mkoani kwake, itakua nafasi nyingine ya kuendelea kutembelea Tanzania zaidi na zaidi kuangalia mambo mengi ambayo hatukuyajua,” Bi. Breeveld alisema.

Naye Bibi Tullah Mloge ambaye ni Mratibu wa Ubia wa Kituo cha SAGCOT, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa dhamira yake ya kusaidia vikundi vya kinamama wakulima na kuina vinanufaika na shughuli wanazofanya katika mnyororo wa thamani wa mazao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...