Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Taasisi ya Sekta Binafsi ya Tanzania (TPSF); Bodi ya Uwekezaji ya Mauritius (BOI), Taasisi ya Biashara na Viwanda ya Mauritius (MCCI) pamoja na Shirika la Serikali la Viwanda Vidogovidogo la Mauritius (Enterprise Muritius kinaratibu Kongamano la Biashara na Uwekezaji Kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika tarehe 23 Machi, 2017 Port Louis, Mauritius. 

Lengo la kongamano hili ni kuwakutanisha ana kwa ana wafanyabiashara/wawekezaji wa nchi hizi mbili ili kujadiliana fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji zitakazowezesha kuanzisha na kuendeleza miradi ya viwanda, kupata wabia wa kuleta mitaji ya biashara, tekinolojia pamoja na kupata masoko.

Sekta zilizolengwa ni kilimo, viwanda vya sukari, viwanda mawasiliano, usafirishaji, uvuvi, ujenzi, utalii, taasisi za fedha, elimu, bima na afya.

Tunategemea Tanzania itaongeza thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka nje (FDI) iwapo makampuni ya wafanyabiashara kutoka Mauritius na Tanzania yatakubaliana kufanya biashara na kuwekeza Tanzania. TIC inapenda kutumia fursa hii kuwatangazia wafanyabiashara nchini kushiriki kongamano hili.

Wafanyabiashara watakaopenda kushiriki kongamano hili watahitajika kujiandikisha TIC kabla ya tarehe 20 Machi, 2017 kwa (Bi. Latiffa Kigoda simu. 0715734444 /latiffa.kigoda@tic.co.tz) au (Bw. Ayoub Magarya simu no. 0654862931/ ayoub.magarya@tic.co.tz). Programu ya kongamano itatumwa kwa washiriki mara baada ya kuthibitisha ushiriki wao.

Imetolewa na OFISI YA UHUSIANO,
KITUO CHA UWEKEZAJI
PO Box 938, Dar Es Salaam 
Website: www.tic.co.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...