Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameagiza kusitishwa
mara moja kwa shughuli zote za kibinadamu kando kando ya Vyanzo vya maji.
Rai hii imetolewa leo na
Waziri Makamba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika
Mkoa wa Pwani eneo la Mto Mpiji ambao umeathirika kutokana na Uchimbaji wa
mchanga na mmomonyoko wa ardhi unaohatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Waziri Makamba amemuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu kuwaondoa watu wote
waliojenga pembezoni mwa Mto Mpiji na kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ndani
ya siku 30. " Mkurugenzi hakikisheni kuwa wakazi hao waliovamia eneo la
mto huu na kujenga makazi yao ya kudumu wanaondolewa mara moja"
Alisisitiza Waziri Makamba.
|
Baadhi ya nyumba zilizopo Mpigi darajani ambazo
zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa ndani ya mita sitini kutoka katika
chanzo cha maji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) amegiza wenye nyumba hizo wabomoe kwa
gharama zao wenye.
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na wananchi wa eneo la Mpigi
darajani (hawapo pichani) na kusisitiza katazo la kufanya shughuli zozote za
kibinadamu ndani ya mita sitini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Bagamoyo Bi. Fatuma Latu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) alipotembelea Mamlaka ya Usafi na
Mazingira Chalinze kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika mto Wami.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...