Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo na Warsha ya Wanahabari za michezo  juu ya maadili ya utangazaji kwenye radio na Televisheni na kuzingatia taaluma.
 Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Superdoll, Jamal Baiser akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watangazaji wa waandishi wa habari za michezo
 Mwalimu Alex Kashasha akitoa mada juu ya kuwaleta wasikilizaji na watazamaji kuwa sehemu ya watu waliopo uwanjani pasipo kusababisha mfarakano wa moyo na kulaumu marefa na wachezaji kutokana na aina ya utangazaji tulionao sasa
 Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. NAWAPONGEZA WAANDAAJI WA SEMINA HIYO. KWA UPANDE WA MAONI YANGU-SEMINA KAMA HIZO ZISITOLEWE DAR ESSALAAM PEKE YAKE, ZITOLEWE NA MIKOANI VITUO NI VINGI NA CHANGAMOTO NI NYINGI. KWA MFANO KATIKA KITUO KIMOJA CHA RADIO WALIKUWEPO WATANGAZAJI WAWILI WA KIPINDI CHA MICHEZO CHA AJABU WAO WENYEWE WAKAAMUA KUJITANGAZA KUWA MMJOA NI MPENZI WA SIMBA NA MWINGINE YANGA. CHA AJABU WANAJIKUTA WAKIJIPONDA WAO WENJEWE BAADA YA KUFANYA KAZI. KWA MFANO HUU NASHAURI WASITUSAHAU MIKOANI KWANI WAPO WATANGAZAJI WENGI WANAHITAJI MSAADA WA KUKUMBUSHWA WAJIBU WAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...