WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama hicho utakapokamilika.

Pia Waziri Mkuu amevunja Bodi ya WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania – TTB kwa sababu ya kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo jioni (Alhamisi Machi 16, 2017) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.

Viongozi wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

“Kuanzia sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara (katikati) na Makamu wake, Msafiri Ngassa wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamis Issah (kulia) kuelekea kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto) wakiwa kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...