Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.

Na: Lorietha Laurence – WHUSM, Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuzisoma, kuzielewa na kuzifanyia kazi sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na ile ya Haki ya kupata Taarifa ya mwaka 2016 ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuuhabarisha umma.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ambapo licha ya kuwataka kuzijua sheria hizo pia amewataka kuwa wabunifu kuendana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia katika utendaji kazi wa kila siku.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.

Aidha aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hizo mbili kutatengeneza daraja litakalounganisha na kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa wananchi. “Ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano kuzijua na kuzitendea kazi sheria hizi ili kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano baina ya serikalini na umma hivyo kuondoa ugumu uliokuwepo hususani katika kupatikana kwa taarifa muhimu kwa wananchi” alisema Waziri Nape.

Aliongeza kwa kufafanua kuwa endapo utekelezaji wa sheria hizi mbili muhimu utasimamiwa na kuzingatiwa basi kutakuwepo na matokeo chanya ya kiutendaji na hivyo kuleta mafanikio makubwa yanayotarajiwa na umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...