Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, "Dar Young Africans" wameshindwa kutamba kwenye kiwanja cha nyumbani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco ya Zambia uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza saa 10 alasiri, ilikuwa ni Yanga iliyowachukua dakika 38 kuandika goli  la kwanza kupitia kwa Simon Msuva akiifungia goli la kuongoza akipokea pasi ya Justine Zulu.

Yanga walishindwa kutumia nafasi walizozipata na mpaka kufikia mapumziko Yanga wanaenda wakiwa kifua mbele.

Kipindi cha Pili kinaanza kwa kila upande kulishambulia goli la mwenzake, hali iliyompelekea Kocha George Lwandamina kufanya mabadiliko kwa kumtoa Donald Ngoma na Thaban Kamosoku na kumuingiza Juma Mahadhi na Emanuel Martin.

Katika Dakika ya 82, Atram Kwame anaisawazishai Zanaco wakitumia mwanya wa kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga.

Mpaka dakika tisa zinamalizika Yanga 1-1 Zanaco ambapo mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa kati ya Machi 17-19.
 Nahodha wa Timu ya Zanaco, Ziyo Kola akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Beki wa Yanga, Hassan Kessy akikabiliana na Mshambuliaji wa Timu ya Zanaco ya nchini Zambia, Kennedy Musonda, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiruka 'Samasoti' mbele ya mashabiki wa Yanga, baada ya kuifungia timu yake goli, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiangalia wa kumpasia mpira, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Juma Mahadhi wa Yanga, akijarimu kupiga mpira wakati wa shambulizi katika lango la Timu ya Zanaco, wakati wa mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...