THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BREAKING NYUZZZZZ......: MAHAKAMA YAMUACHIA HURU ASKOFU GWAJIMA

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya kutumia lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinari Pengo.

Askofu Gwajima ameachiwa huru chini ya kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha ameifuta kesi hiyo baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashahidi kwa takribani miaka miwili.

Kabla ya kufutwa kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Joseph Maugo aliieleza mahakama hiyo kuwa leo kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba hawana shahidi hivyo wanaomba ahirisho lingine.


Hakimu Mkeha amesema kwa muda wa miezi 14, upande wa mashitaka umeweza kuleta shahidi mmoja pekee hivyo anafuta kesi hiyo.

Awali, katika shauri lililopita aliutaka upande wa mashitaka kuhakikisha wanaleta mashahidi kusikiliza kesi hiyo.

Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Machi 16 na 25, mwaka jana maeneo ya Tanganyika Packers Kawe Askofu Gwajima alitumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Askofu Pengo.

Inadaiwa alimuita; Ni mpuuzi mmoja mjinga mmoja asiyefaa mmoja anaitwa Askofu Pengo aliropoka sijui amekula nini mimi naitwa Gwajima namwita mpuuzi yule mjinga yule  na kuonesha Pengo ni mtoto mpuuzi na mwenye akili ndogo na kwamba maneno hayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani.