Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na hata nje ya nchi. 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe, alipokuwa akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo. 

Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan katika suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo nimepata picha kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri muandae dira endelevu kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe. 

Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma. 

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe wake iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali, umeonesha nia yakuleta walimu wa Whushu. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt Harrison George Mwakyembe akizungumza katika mahafali ya Chuo cha waalimu Michezo Malya Jijini Mwanza. 
Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw. Yusufu Omary Singo akitoa nasaha kwa wahitimu wa mafunzo katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa kozi fupi ya uwalimu wa michezo yaliyofanyika Chuo cha Mwaalimu wa Michezo Malya Jijini Mwanza. 
Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wa kozi fupi ya uwaalimu wa michezo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Dkt. Harrison George Mwakyembe alipokuwa akizungumza nao katika mahafali ya Chuo hicho Jijini Mwanza. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...