Mchezaji wa timu ya Dar City, Shadrack Nsajigwa akiondoka na huku akisindikizwa na Mchezaji wa Timu Boko Veterans wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo Dar City ilishinda mabao 3-2, kupitia kwa wachezaji wake Makocha Tembele na Salvatory Edward. Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji mbalimbali waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Tanzania miaka ya nyuma pamoja na .
Kiungo hodari wa Dar City, Shaffih Dauda akiwania mpira na Mchezaji wa Timu Boko Veterans wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo Dar City ilishinda mabao 3-2, kupitia kwa wachezaji wake Makocha Tembele na Salvatory Edward. Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji mbalimbali waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Tanzania miaka ya nyuma pamoja na baadhi ya wadau wa soka na wanahabari.
Kiungo wa Timu ya Dar City, Tippo Athuman al maarufu Zizzou ambaye ni muasisi wa timu hiyo, akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Boko Beach Veterans, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. 
Nahodha wa Timu ya Boko Beach Veterans, John Dilinga a.k.a Dj JD akiajiandaa kuachia shuti.
Makocha Tembele (katikati) akiwasakata wachezaji wa Boko Veterans, Godfrey Ngonyani (kushoto) na John Dilinga 'Dj Jd'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...