THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC JUMA HOMERA AFANIKIWA KUANZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA, TUNDURU.


AOMBA WANANCHI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAMUUNGE MKONO KUFANIKISHA AZMA YAKE

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera ameazisha ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya, lengo la kuanzisha kituo hiki ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya Tunduru huzidiwa na wagonjwa kushindwa kupata matibabu kwa wakati.

Kata ya Nakayaya ipo umbali wa kilomita tano toka Tunduru mjini, kituo hiki kinatarajiwa kuhudumia kata ya Nakayaya, Masonya, Mlingoti na Nandembo/ Tarafa ya Mlingoti na Nampungu pamoja na maeneo ya jirani.

DC Homera alianzisha mchakato huo kwa kutafuta eneo la kujenga kituo na mara baada ya kupata eneo alimtafuta mchora ramani wa kituo cha afya na mara baada ya kupata ramani alitafuta vijana wa kusafisha eneo na hivi sasa mchanga wa kuanzia ujenzi upo eneo la ujenzi.

Jumla ya mifuko mia tatu ya saruji imepatikana, fedha bado zinakusanywa toka kwa wananchi, wafanyabiashara, makundi ya Vijana mbalimbali wa wilaya ya Tunduru,hivyo anawaomba wadau wengine wamuunge mkono.

Jumla ya matofali elfu thelathini zina hitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha afya na zoezi la ufyetuaji utaanza hivi karibuni, vikundi mbalimbali vya vijana vinatarajia kuweka kambi ili kufanikisha zoezi hili.

Aidha, Dc Homera amewaomba wananchi wote waungane kufanikishe ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya na hivi karibuni atatoa utaratibu wa kujitolea.

"Tunduru Mpya itajengwa na wenye moyo, wananchi wenzangu wa Tunduru nawaomba tuungane kujenga kituo hiki cha afya na hivi karibuni nitatoa utaratibu wa kujitolea kila mmoja Wetu, tumtangulize Mungu mbele tutafanikiwa kwa ushauri namna ya kufanikisha namba zangu ni +255759814088. Tumuuge mkono Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania nasi kwa upande Wa wana Tunduru tuna wajibika".
Mchoro wa kituo hicho kitakavyoonekana mara baada ya kukamilika.


Muonekano kwa nje itakavyokuwa.

Sehemu mbalimbali ndani ya kituo hicho kitakavyoonekanaKuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Unknown Anasema:

    Hongereni sana kwa hatua mliofikia. Ila swali la jkizushi, mgonjwa wa wodini anafikaje kwenye jengo la upasuaji? Na wa kwenda mortuary anapitishwa parking lot?

  2. Fred Mutah Anasema:

    Position ya mortuary ni mbaya sana katika plani hii.....hebu imagine unafika reception ukiangalia pembeni unakutana na au unaona wafu wanatolewa moruary.....
    kwa kawaida mortuary inakuwa nyuma au pembeni ikiwa imeunganishwa na wodi au chumba cha upasuaji..na ni vizuri shuguri zinazoendelea ndani ya motuary zisiwe zinaonekana wazi kwa watu walio wengi hospitalin..hii ni kuwapa wagonjwa matumain ambayo wakati mwingine yanasaidia katika tiba...kwa kuwa ni mchoro tu bado hamchelewa please ondoeni mortuary mbele ya Hospitar/kituo cha afya....pamoja na hayo Mortuary ni muhimu sana katika design ya hospital au health center...