MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi jana jioni amekarimu wageni wafanyabiashara wa Ufaransa waliopo katika wiki ya Ufaransa nchini. Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa 50 ya Ufaransa wakiongozwa na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Zoro. 

Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hicho, Dk. Mengi alisema katika hoteli ya Serana ikiwa ni njia mojawapo ya kuonesha shukurani kwa wafanyabiashara hao kuamua kuja nchini kuwekeza. Alisema jioni hii ya leo hana maneno mengi ya kuzungumza zaidi ya kuwakarimu wageni hao ambao ni muhimu sana kwa Watanzania, sekta ya uchumi na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hafla maalum ya chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili ya ugeni huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak.(Picha zote na Thebeautytz.com)

 “Ujio wenu nchini ni wa kufurahisha sana, utatunufaisha taifa na nyie pia hii ndiyo tunayoita win win situation” alisema Dk Mengi na kuongeza kuwa ujio wao utasaidia kujenga uwezo wa teknolojia wa taifa hili. Aidha alisema kwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yenye msuli wa kiuchumi kuwa rafiki wa Tanzania kutasaidia Watanzania kuwa na rafiki mwenye uwezo wa kuwasaidia kuwa na uwezo pia. Alisema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa una historia yake na kwamba kwa sasa utaendelezwa zaidi. Aliwatakia wageni wake chakula chema.. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akiwakaribisha wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa kwenye halfa ya chakula cha jioni aliyoiandaa maalum kwa wafanyabiashara hao katika hoteli ya Serena jijini Dae es Salaam. 

 Mgeni rasmi ambaye alikuwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema kwamba amefurahishwa sana na ukarimu wa Dk Mengi na kusema kwamba yeye anaamini biashara na urafiki ni kitu muhimu katika kuimarisha mahusiano. “ …Business and friendship goes Together..” alisema balozi huyo kwa lugha ya kiingereza na kuongeza kwamba kutokana na chakula hicho anaamini kwamba urafiki wa watu wa Ufaransa na Tanzania si wa kubahatisha unakua. Katika chakula hicho miongoni mwa wa kampuni zilizofika ni Airbus, Siemens, General electrical na kadhalika. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi na Mgeni rasmi Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak (kulia) wakiendelea kupokea wageni mbalimbali kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyoandaa kwa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi akitoa neno la ukaribisho kwenye 'cocktail' kabla ya kushiriki chakula cha jioni na wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...