Na  Bashir  Yakub.

Kwa  mujibu  wa  sheria  ya usajili  wa  ardhi  sura ya  334   ipo  aina   ya  mikataba  ya  pango  ambayo  baada  ya  kuwa  imeingiwa  kati  ya  mpangaji  na  mwenye  nyumba/eneo  ni  lazima  isajiliwe.

  Mikataba  ya  aina  hiyo  isiposajiliwa  inakuwa   haijakidhi  vigezo  vya  kisheria  na  hivyo  kubatilika.

Aidha  pango  huhusisha  shughuli  mbalimbali.  Yapo  mapango  kwa  ajili  ya  biashara  maduka,  bar, mahoteli n.k.  na  pia  yapo  mapango  kwa  ajili  ya  makazi. Iwe  umepanga  kwa  ajili  ya  biashara  au  makazi  madhali  aina  yako  ya  upangaji  inahitaji  kusajiliwa  kisheria  basi  huna budi  kufanya  hivyo  ili  uhalali  wa  pango lako  upatikane.

Kabla  ya  kuona  aina  ya  mikataba  ya  pango  ambayo ni  lazima  kusajiliwa  ni  vyema  kujikumbusha  kidogo  kuhusu  haki  za  mpangaji.

1.HAKI   ZA  MPANGAJI.
( a ) Haki  ya  kutoingiliwa  na  mwenye  nyumba  ili  kumpa  uhuru mpangaji   kufurahia  pango  lake.
( b ) Haki  ya  kumpa  taarifa(notice)  mapema  mpangaji  ikiwa mwenye nyumba  anataka  kukagua  nyumba/eneo  lake.
( c ) Haki  ya  kutoondolewa  au  kusitishiwa  mkataba  mpaka  baada ya  kupewa  taarifa  maalum( notice) .
( d ) Haki  ya  kuambiwa  ukweli  kuhusu  hali  ya  nyumba kabla  ya  kusaini  mkataba  wa  pango. Mfano  kuambiwa  ikiwa  eneo  linajaa  maji  kipindi  cha  mvua, kuambiwa  ikiwa  nyumba  inavuja n.k.
( e ) Haki  ya  kukataa  sharti  lolote  ambalo  linalenga kuminya  uhuru   wa  mpangaji  au  linalovunja  sheria  yoyote  ya  Tanzania.
( f ) Haki  ya  kupewa  taarifa  mapema(notice)  kabla  ya  kupandisha  kodi  ya  pango.
( g )  Haki  ya  kupewa  taarifa  mapema(notice)   kabla  ya  kubadilisha  sharti  lolote  katika  mkataba  wa  pango.
         
   KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...