Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ndugu Andrew W. Massawe yuko mkoani Iringa kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu; ambapo pamoja na mambo mengine anatazamiwa kushuhudia sherehe za uzinduzi wa utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi na kuzinduliwa kwa kampeni ya Usajili wa wananchi na wageni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoishi mkoani humo.
Katika ziara yake; leo amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye amemweleza Mkurugenzi huyo hatua kubwa ambayo Wilaya yake imefikia mpaka sasa katika kuwasajili wananchi, ambapo takribani asilimia 60 ya wananchi wameshasajiliwa, kuchukuliwa alama za vidole na baadhi Vitambulisho vyao kuzalishwa, mbali na kukamilika kwa zoezi la kuwasajiliwa Watumishi wa Umma.
 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Mufindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndugu Andrew W. Massawe
 Ndugu George Mushi Afisa Usajili Mkoa wa Iringa (RRO), akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA,  Ndugu Andrew W. Massawe kuhusu vifaa vinavyotumika kwenye usajili wa wananchi alipotembelea ghala la kuhifadhi vifaa wilayani Mufindi
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA  Ndugu Andrew W. Massawe akiwa na Kanali Hamisi Maiga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mafinga namba 841, wakati alipotembelea kambi hiyo.
 Mtendaji wa Kata ya Boma; Joseph Kiwele akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la usajili wananchi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA  Ndugu Andrew W. Massawe. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...