Na  Bashir  Yakub
Transfer  ni  kubadilisha  hati  au  leseni  ya  makazi  kutoka  jina  la  mmiliki  wa awali  kwenda  kwa  mmiliki  mpya.  Transfer  inaweza  kufanyika  kutokana na mauzo, kupewa  zawadi, fidia, n.k.  Kwahiyo  kuzuia  transfer  ni  kuzuia   kubadilishwa  kwa  hati  kutoka  mmiliki wa  awali  kwenda  mmiliki  mpya. Mara   nyingi  tumezoea   kuzuia   transfer  kwa  kutumia  mahakama ( court  injuction).
Sasa  yatupasa tufahamu kuwa  ipo  njia nyingine  nyepesi  ambayo  haihusishi  mahakama.  Ni  njia  ya  maombi  kwa  kamishna  wa  ardhi   kwa  mujibu  wa  Sura  ya  113 ,  sheria  ya ardhi ,namba  4, ya mwaka  1999  vifungu  vya  38, 39  na  41 . Kabla  ya kuona  ufanyeje  kutumia  njia  hii ni  vema  tuone    mazingira  ambayo   yakikutokea unaweza  kutumia  hiyo  njia.

1.HAYA  YAKITOKEA  UNAWEZA  KUPELEKA  MAOMBI  KWA  KAMISHNA.
( a ) Mme  wako  au  mke  wako  ameuza   kiwanja  au  nyumba  yenu  na  kuna  namna  ambavyo  mauzo  hayo   unadhani  sio  halali  kwasababu  yoyote  ile  ya  kisheria pengine ya  kutokushirikishwa,  au  kushirikishwa  lakini  baadae  kunyimwa  haki  yako  kwa  mujibu  wa  makubaliano au  vinginevyo. Lakini   wakati  huo   unadhani  huna  la  kufanya  kwakuwa  mauzo  tayari  yamefanyika  na  pengine  hata  wewe  ulishasaini.
( b ) Una  maslahi  na  haki  katika nyumba/kiwanja  cha  mirathi .  Mali  hiyo  imeuzwa  bila  wewe  kushirikishwa  au  umeshirikishwa  lakini  haki  zako  za  msingi  hazikuzingatiwa  au  namna  nyingine  yoyote  ambayo  kwayo  unahisi  mchakato  haukwenda  sawa.  Lakini   wakati  huo   unadhani  huna  la  kufanya kwakuwa  mauzo  tayari  yamefanyika  na  pengine  hata  wewe  ulishasaini.
( c ) Umemuuzia  mtu  nyumba/kiwanja  lakini  amekataa  kutekeleza  baadhi  ya  makubaliano  ya  msingi yaliyo  katika  mkataba  wenu  wa  mauziano  na  sasa  anafanya  mchakato  wa  kubadili  hati.
( d ) Na mazingira  mengine  yoyote ambayo  tayari  nyumba/kiwanja  kimeuzwa  lakini  ukaona  kuna  haja  ya  kuzuia  mchakato  wa  kubadilishwa jina  la  mmiliki  ili  baadhi  ya mambo yawekwe  sawa  kwanza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...