Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo.
Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa. 

"Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho harafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachi mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy.
Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikai huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.
"Ukiusikia huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana, haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule harafu unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine, nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy 

Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy (kulia) na Msanii Roma Mkatoliki
Courtesy of MCL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...