Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 
Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu (Sumatra) pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji wamekubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliotakiwa kuanza kesho.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitisha huko kunatokana na kikao na waziri mwenye dhamana, Profesa Makame Mbarawa juu ya kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki.
 
Amesema kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea usafirishaji.
 
Ngewe amesema kuwa baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kupeleka bungeni.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Abdallah Mohamed amesema wamekubaliana na Sumatra mambo ambayo hayakuwa sawa warekebishe katika kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
 
Amesema wasipokubaliana baada ya siku 14 watarudi katika mkutano mwingine kwa kila mmoja namna gani ya kuweza kutengeneza sheria ambazo haziathiri upande mmoja.Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala , Kasmat Jaffer amesema suala ambalo limekuwa mwiba ni kosa la kufungwa pamoja na faini hali ambayo wameona ni bora kuachana na biashara hiyo.


: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.

Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea hatua ya kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.

Waandishi wa habari wakiwasikiliza viongozi wa vyama vya usafishaji nchini wakati wakielezea hatua ya kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...