Efm redio 93.7 kituo bora Tanzania, kinachokua kwa kasi kwa matangazo pamoja na ubunifu kimetimiza miaka mitatu sasa tangu kuanzishwa kwake. Redio hii imekua ikitangaza habari mbalimbali za kijamii, kiuchumi, pamoja na michezo kwa lengo la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wasikilizaji wake.
Efm imejitwalia tuzo ya ubunifu ya Tanzania leadership Award kwa miaka miwili mfululizo, kwa kubuni matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakiiwezesha jamii kujikwamua kimaisha kwa kugawa pikipiki, magari ya biashara (shikandinga), fedha taslimu, maakuli (kapuu ya sikukuu) pamoja na mafuta kwa madereva wa vyombo vya usafiri pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wanawake.
Pia imeanzisha kampeni mbalimbali za kutia hamasa katika jamii ikiwemo (kampeni ya Mti wangu) yenye lengo la kumhamasisha kila mtu kupanda mti, na kufanya mazoezi mtaani pamoja wanafunzi wa vyuo kupitia kikundi cha Efm jogging club.
Redio hii imejipatia umaarufu sana kwa kuukuza muziki wa singeli ambao awali ulidharauliwa na kukosa hadhi, Licha ya kuukuza redio hii imeusafisha kwa kuwaelimisha wasanii wa muziki huo kwa kuwapa semina mbalimbali ikishirikiana na taasisi mbalimbali kama BASATA, COSOTA, TCRA, na TRA hadi sasa muziki huu unachezwa na kutambulika na redio nyingine ndani na nje ya Tanzania.

Aidha katika kuendeleza mafanikio yake, Redio hii imeongeza masafa yake katika mikoa Tisa ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza, Mbeya, Mtwara, Singida, Tanga, Tabora, Manyara (Babati), Kilimanjaro (Moshi), na Kigoma pamoja na kuanzisha rasmi kituo dada cha Televisheni kinachofahamika kama TV-E ambayo kwa sasa inafanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...