BOHARI ya Dawa (MSD) imeshiriki Jukwaa la Biashara, lililoandaliwa na Kampuni ya magazeti ya TSN, jijini Mwanza. Katika Jukwaa hilo, MSD pia imeshiriki maonesho ya vifaa tiba.

Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo jijini Mwanza jana Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (pichani) amewahakikishia wadau wa Mwanza fursa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha dawa nchini, endapo watakidhi ubora unaohitajika.

Amesema, hatua hii inafuatia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi na taasisi za Umma katika uwekezaji.

Bwanakunu amefafanua kuwa uanzishwaji wa viwanda nchini utapunguza gharama za uagizaji dawa na vifaa tiba toka nje ya nchi, kuokoa fedha za kununua nje,kusafirisha,kugomboa na kupata dawa kwa muda mfupi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...