Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imendelea kuwajengea uwezo madaktari wa ndani na nje ya hospitali kwa kufanya upasuaji wa njia ya matundu madogo (laparoscopic surgery).

Miongoni mwa madaktari walioshiriki kwenye upasuaji huo ni kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.

Lengo ni kuwaongezea ujuzi madaktari hao ili waendelee kufanya upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo kwa wagonjwa mbalimbali.
Upasuaji huo unafanywa na madaktari wa muhimbili kwa kushirikiana na Daktari Bingwa aliyebobea katika magonjwa ya kinamama na uzazi, Profesa Rafique Parkar ambaye amekuwa akifanya upasuaji huo nchini Afrika Kusini, Kenya na nchi mbalimbali barani Afrika.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama na Uzazi, Vicenti Tarimo wa hospitali ya Muhimbili amesema wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji na kwamba wengine watatu walikuwa wakiendelea kufanyiwa upasuaji huo leo.
 Daktari Bingwa aliyebobea katika Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar akifanya upasuaji wa kutumia njia ya matudu madogo kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. 
 Baadhi ya madaktari kutoka katika Hospitali za umma na binafsi nchini wakifuatilia mubashara upasuaji wa njia ya matundu madogo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...