Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akifanya mazoezi na vikundi vya michezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kabla ya kufungua Bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya mazoezi na vikundi vya michezo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara kabla ya kufungua Bonanza kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanamichezo wa vikundi mbalimbali kutoka Zanzibar na Tanzania Bara mara baada kiongozi huyo kufanya mazoezi ya viungo na wanamichezo hao katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka wanamichezo hao pamoja na wananchi hapa nchini kwa ujumla, kudumisha mazoezi zaidi ili waweza kupata afya bora.
Msoma Risala wa Kikundi cha Michezo cha Island Erercise Club cha mjini Unguja, Zanzibar, Ally Mussa, ambacho ndio waratibu wa Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka Visiwani humo pamoja na Tanzania Bara, akitoa historia fupi ya kikundi hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, kabla ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kukariboishwa kuzungumza na mamia ya wanamichezo ambao walifanya mazoezi mbalimbali katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar leo. Wapili kulia ni Bregedi Kamanda KV101 kambi ya nyuki, Kanali Fadhili Nonda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiumwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda katika eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Zanzibar, mara baada ya kufanya mazoezi ya viungo katika Bonanza la Vikundi vya Michezo kutoka visiwani humo pamoja na Tanzania Bara. Masauni aliwakilisha Makamu wa Rais, Sami Suluhu katika sherehe hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...