THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Tamasha la muziki "Karibu" latangaza nafasi za ushiriki kwa wasanii

Uongozi wa Tamasha la muziki la Karibu wakishirikiana na Legendary Music Entertainment wametangaza nafasi kwa wasanii wa muziki na vikundi mbalimbali vya muziki kuomba nafasi za kutumbuiza kwenye tamasha la 4 kwenye uwanja wa Mwanakalenge, Bagamoyo

Tamasha hilo lenye hadhi ya kimataifa litakua la siku tatu mfululizo litakalofanyika tarehe 3-5 Novemba mwaka huu. Watumbuizaji katika tamasha hili ni wasanii wa kimataifa kutoka Africa, Ulaya, America na Asia ambapo watumbuizaji wote hutumbuiza mubashara asilimia 100. Tamasha hili huwapa wanamuziki nafsi ya kuonesha kazi zao za muziki sambamba na kuuza kazi zao.

Kupitia tangazo linalopatikana kupitia mtandao wa www.karibumusic.org inaonesha mwisho wa kufanya maombi hayo itakua tarehe 31 Augusti mwaka huu. Maombi hayo yafanyike moja kwa moja kupitia fomu inayopatika kwenye tovuti ya karibu.

Amarido Charles Mkurugenzi wa Tamasha amesema tamasha linalenga kuonesha kazi za muziki, kukuza sanaa, kutangaza utalii na tamaduni za kitanzanzia na Afrika kwa ujumla. Pia tamasha hilo hutoa fursa kwa wasanii wa ndani ya Nchi kupanua wigo wa mawasiliano na wanataaluma wengine kwenye tasnia ya sanaa ya muziki.

Tamasha la muziki la karibu limetajwa kwenye orodha ya matamasha ya kuvutia na muhimu dunianiani na World Music Oasis Sweden. 

Tamasha la Karibu ni tamasha la kimataifa linaloandaliwa na watanzania wenye mapenzi na muziki, sanaa na utamaduni. Tamasha hili hufanyika Bagamoyo, mji wa kihistoria ya biashara ya watumwa ambao walisafirishwa kupitia Bahari ya Hindi mpaka soko la watumwa Zanzibar kabla ya kusafirishwa kwenda Asia na sehemu mbalimbali.