Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kesho inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya maombi ya Serikali ya Marekani ya kuwataka raia watatu wa Tanzania wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya kama waende nchini humo kusikiliza tuhuma hizo ama la.

Wajibu maombi wanaotuhumiwa nchini humo ni mfanyabiashara bilionea, Ally Khatib Hajj maarufu kama Shkuba, mfanyabiashara Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam maarufu Tiko.
Katika maombi hayo, serikali inaiomba mahakama itoe amri ya kuwakamata na kuwazuia watuhumiwa hao ambao ni wajibu maombi ianzishe utaratibu wa kuwasafirisha kwenda nchini humo. 

Uchunguzi unaonyesha kuwa mshtakiwa Shkuba, na wenzake walihusika kwenye njama za kusambaza zaidi ya kilo moja ya dawa za kulevya aina ya Heroine ambazo zimezuiliwa nchini humo.
Maombi ya Marekani, yaliyosikilizwa mbale ya hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, yaliwasilishwa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe kupitia, Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki.
Wajibu maombi wanatetewa na jopo la Mawakili watatu, wakiwemo Edson Ndusyepo, Majura Magafu na Adinan Chitare.
Wakati wa usikilizwaji Kakolaki alieleza kuwa Waziri wa sheria wakati huo Mwakyembe alipelekewa maombi ya kutakiwa kwa wajibu maombi hao ambapo Aprili 4, mwaka huu mahakama ilitoa amri ya kukamatwa kwao na Aprili 6 walikamatwa na jana walifikishwa mahakamani hapo ambapo maombi hayo yaliwasilishwa.
Kakolaki ameendelea kudai kuwa maombi ya kuwasafirisha wajibu maombi ni halali kwani kumekuwa na mahusiano ya Tanzania kubadilishana wahalifu na nchi za Ulaya tangu enzi za ukoloni wakati Tanzania inaitwa Tanganyika.


Wajibu maombi ambao wanatuhumiwa nchini Marekani ambao ni mfanyabiashara bilionea, Ally Khatib Hajj maarufu kama Shkuba (fulana nyekundu), mfanyabiashara Idd Mafuru (wa pili kulia) na Lwitiko Emmanuel Adam maarufu Tiko (kulia) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.a

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...