THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Vijana waaswa kuchangakia fursa mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Vijana wametakiwa kujitokeza katika fursa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi. Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Manispaa ya Temeke, John Bwana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mradi wa vijana wajibika unaotekelezwa na Restless, amesema kuwa vijana wamekuwa nyuma katika fursa zinazotolewa na serikali na mwisho wa siku wanabaki wakilalamika bila kujua kuwa wao ndio kikwanzo. 

Amesema mfuko wa vijana wa kuwakopesha umetoka kwa kuwasaidia vijana lakini idadi ya waliojitokeza ni ndogo na baadhi yao wengine walifatilia siku ya kwanza na kuambiwa kufanya taratibu za vikundi hawakuweza kurudi ili waweze kufanya utaratibu wa mkopo huo. Aidha amesema vijana wa Temeke wako nyuma kimaendeleo  ukilinganisha na manispaa zingine zilizo katika jiji la Dar es Salaam katika uchangamkiaji wa fursa mbalilmbali zinavyojitokeza.

Bwana amesema kuwa vijana wanatakiwa kupewa elimu ili waweze kujenga uchumi wa taifa kupitia mikopo mbalimbali wawe wanajitokeza na mawazo yao kufanyiwa kazi kwa vitendo.

Nae Meneja wa Mradi huo, Oscar Kimaro amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa mitatu  ya Iringa , Morogoro pamoja na Dar es Salaam ambapo Restless wamefanya utafiti wa ufatiliajia wa mkopo wa kundi la vijana wanaopewa ambapo wamebaini vijana wanashindwa kunufaika na mkopo huo kutokana na changamoto mbalimbali katika maeneo yao. 

Kimaro amesema kuwa kwa maafisa wa maendeleo ya jamii wana kazi ya ziada katika kutoa elimu ili mkopo wa serikali kuweza kuwafikia vijana na kuweza kuondokana na umasikini. Wakili wa Uwajibikaji na Utetezi kwa Vijana wa Restless, Situ Magenge amesema walifanya utafiti na kubaini waliopata mkopo ni zaidi ya umri uliowekwa na baadhi ya kata zingine katika manispaa ya Temeke vijana walisema kitu hicho hawa kijui juu ya utekelezaji wake.

Afisa Maendeleo ya Manispaa ya Temeke, John Bwana akizungumza na maafisa maendeleo wa Kata juu ya mkopo wa vijana katika uzinduzi wa ripoti mradi wa wajibika vijana wa ufatiliaji wa mkopo kwa vijana chini ya Restless jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Vijana wa Manispaa ya Temeke, Anna Marika akizungumza watendaji juu utekelezaji wa mkopo kwa vijana katika uzinduzi wa ripoti mradi wa wajibika vijana wa ufatiliaji wa mkopo kwa vijana chini ya Restless jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Uwajibikaji na Utetezi kwa Vijana wa Restless, Situ Magenge (aliyesimama kushoto) akisoma ripoti ya utekelezaji wa mkopo wa vijana katika mikoa mitatu ya Iringa, Morogoro pamoja na Dar es Salaam.
Meneja wa Mradi, Osca Kimaro akizungumza na watendaji wa kata wa Manispaa ya Temeke katika uzinduzi wa ripoti mradi wa wajibika vijana wa ufatiliaji wa mkopo kwa vijana chini ya Restless jijini Dar es Salaam.