Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi 

Wananchi wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kujenga uchumi wa viwanda nchini. 

Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi na kusema kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni ule utakaolifanya taifa kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za viwanda vya mataifa mengine. 

“Tanzania tumeazimia kutoka katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao utahusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta binafsi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan katika uwekezaji mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na upatikanaji wa rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi Iddi. 

Aidha Mhe. Balozi Iddi amesema kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika kujenga na kuendeleza viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda unaanza kwa jitihada za wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa wanazozalisha kila siku katika maeneo yanayowazunguka. 
: Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Watumbuizaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...